Thursday, December 31, 2009

Kwa Heri 2009,Karibu 2010

Leo mungu akipenda tutaumaliza mwaka 2009 na kuingia mwaka mpya wa 2010 saa chacha kutoka sasa.

Hata hivyo kiutendaji mwaka 2009 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwani wadau wa tasnia ya Habari nchini walishuhudia Kagera Press Club ikianzisha gazeti la kiswahili mapema mwezi wa pili baada ya mchakato wa takribani miaka mitano.

Mategemo ya Kagera Press Club,wadau ni kwamba mwaka 2010 ambao ni wa uchaguzi kwa Tanzania ni mwaka mgumu sana kwa upande wa waandishi wa habari kwani ni mwaka ambao baadhi yao madili ya uandishi wa habari uwekwa kando katika kutekeleza majukumu yao.

Tunachukua fursa hii kuwatahadharisha wanachama wa Kagera Press Club kuwa makini katika kutekeleza kazi zao kwa mwaka mzima tnaotarajia kuangia wa 2010.

Tusitegemee wanataaluma wengine kutujengea taaluma yetu,MJENGA NCHI NDIYE MBOBOA NCHI kazi kwenu.

Tunawatakia kazi njema.

Imetolewa na
Mwenyekiti wa Kagera Press Club

Sunday, December 20, 2009

Mwanachama wa Kagera Press Club ashinda Tuzo za Mwandishi Bora 2009

Bw Phinias Bashaya(pichani) ni mmoja wa washindi wa tuzo za mwandishi bora wa mwaka zilizoandaliwa na baraza la habari la Tanzania(MCT) na wadau wengine wa habari nchini.

Bashaya ambaye ni mwandishi wa gazeti la Habarileo alishinda tuzo hiyo kwa upande wa jinsia kufuatia makala ya uchunguzi iliyohusu wakazi wa visiwani vilivyoko katika ziwa victoria upande wa mkoa wa kagera kufuatia kupata ruzuku kutoka mfuko wa kusaidia vyombo vya habari(tmf).

kufuatia ushindi huo bashaya amekabidhiwa tuzo,cheti na computer ndogo katika sherehe zilizozofanyika desemba 19,2009 jijini dar na alikabidhiwa tuzo na Rais wa UTPC Bw Ken Simbaya.
TUTACHAPISHA HAPA MAKALA ILIYOSHINDA TUZO HIYO SIKU CHACHE ZIJAZO.

Kujua kile kilicjojiri na wenghine walioshinda
gonga hapa

Uongozi wa Kagera Press Club na wanachama wengine wanatoa pongezi kwa mwanachama mwenzao kupata tuzo hiyo na wengine wanaombwa kuiga mfano wake.

Thursday, December 17, 2009

Mwandishi unaweza kutoa story yako kupitia video cheki hii

Wapendwa waandishi nimetumiwa video na mtandao wa IJNT ambapo waandishi kuele marekani wanaweza kutumia picha za video kueleza ukweli wa jambo kupitia video.

ebu gonga hapa

Tuzo za Mwandishi Bora Tanzania 2009 Kagera Press Club itaambulia chochote ?

Wapendwa wanachma wa Kagaera Press Club pamoja na wadau wengine wanaosoma blog hii ni kuwa ile siku iliyosubiriwa sana na wadau wa habari ya kutanagzwa kwa waandishi bora wa mwaka 2009 iliyoandaliwa na baraza la Habari Tanzania(MCT) pamoja na vyama vingine vya waandishi na mfuko wa Tanzania Media Fund(TMF) itafanyika desemba 19,2009 katika jiji la Dar Es salaam.

kikubwa ni washiriki wa tuzo hizo kutoka Kagera Press Club waliowasilisha kazi zao za uchunguzi ni watano,mwanamke mmoja.

ngoja tusubiri kama watashinda tuzo husika.

tutawajulisha matokeo kupitia blog hii.

Matokeo ya Uchunguzi wa KPC juu ya matumizi Mabaya ya Fedha Bukoba Vijijini

Mwaka 2008 Kagera Press Club ilifanya uchunguzi juu ya matumizi mabaya ya fedha kwa Halamshauri ya Bukoba vijijini na kubanisha mambo kadhaa.

tumelazimika kuiweka hapa baada ya kuombwa na wadau wetu kufanya hivyo ebu gonga hapa kujua kiliacobanishwa.

Matokeo ya Uchunguzi wa KPC juu ya matumizi Mabaya ya Fedha Bukoba Vijijini

Bohari Kuu ya Mkoa, Jamhuri Road, P.O.Box 1899 Bukoba, Kagera, Tanzania. Tel/Fax 028 2220183,Mob 0754527358 , Email: presskagera@yahoo.com

ZOEZI LA UFUATILIAJI WA FEDHA ZINAZOTOLEWA KWA AJILI YA MAENDELEO YA ELIMU YA MSINGI KATIKA WILAYA YA BUKOBA VIJIJINI

Hii ni nyumba alimopanga Mwalimu Alfred Jeremiah wa Shule ya Msingi Karama kutokana na kukosa nyumba ya kuishi shuleni hapo baada ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu chini ya mpango wa MMEM kukwama kwa sababu za ubadhilifu wa fedha.

YALIYOMO

Utangulizi........................................................................................................ uk. 3

Lengo Kuu......................................................................................................uk. 4

Lengo Mahususi...........................................................................................uk. 4-5

Madhumuni ya PETS

Mantiki ya Zoezi

Njia za Uchunguzi........................................................................................uk.5-6

Matokeo ya jumla.........................................................................................uk.6-7

Vyumba vya Madarasa/ Vifaa

Kamati za Shule

Matokeo Mahsusi ya zoezi la PETS…………………………………………uk.7-15

Udadhilifu wa fedha

Madaraka ya Kamati za Shule

Changamoto……………………………………………………………………...uk.15-20

Mapendekezo……………………………………………………………………..uk.19-22

Hitimisho…………………………………………………………………………..uk 23-24

VIAMBATANISHO

Mwongozo wa Uimarishaji wa Kamati za Shule za Msingi katika Mpango shirikishi, Usimamizi wa fedha na vifaa. Moduli ya pili I

Nakala za madodoso yaliyotumika II

Barua mbalimbali kutoka halmashauri zinazoelekeza matumizi ya fedha III

Nakala ya habari za Magazeti IV

Utangulizi

Taarifa hii inahusu zoezi la ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za Umma (PETS- Public Expenditure Tracking System) zilizopokelewa kwa ajili miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu katika shule zilizoko wilaya ya Bukoba vijijini chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). Zoezi hili pia lilihusu ufuatiliaji wa matumizi ya fedha kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya wanafunzi kitaaluma zinazotolewa kupitia utaratibu wa «Capitation Grant » kwa uwiano wa wanafunzi wa shule husika.

Zoezi hili lilifanyika kutokana na kuwepo kwa tashwishi za matumizi mabaya ya fedha kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba zilizotolewa chini ya Mpango Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM).

Kutokana na taarifa hizo, Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoani Kagera, kwa ufadhili wa Shrilika la Maendeleo la Uholanzi(SNV), kilimteaua Bw Joas Kaijage ambaye ni Mwandishi wa Habari za Uchunguzi na mwanachama wa (KPC), kufanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli wa tashwishi hizo.

Zoezi hili lilifanyika kuanzia June 15 hadi Novemba 1, 2008 na kuhusisha shule 20 za Msingi ambazo ziko kwenye vijiji na tarafa kama inavyooneshwa kwenye jedwali hapa chini. Utafiti huu umefanywa na Bw Joas Kaijage kama mtafiti Mkuu pamoja na watafiti wasaidizi wawili.

Text Box: SHULE KIJIJI KATA TARAFA NTOMA BUTAHYAIBEGA KANYANGEREKO KYAMUTWARA NYARUBALE BULINDA KANYANGEREKO KYAMUTWARA MAIGA BUTAIRUKA MARUKU KYAMUTWARA KATOMA A LUKINDO KATOMA KYAMUTWARA KATOMA B KASHENGE KATOMA KYAMUTWARA RUBALE RUBALE RUBALE RUBALE RUKOMA RUKOMA RUBALE RUBALE KARAMA NSHESHE RUBALE RUBALE NSHESHE NSHESHE RUBALE RUBALE NYAKAJU RUBALE RUBALE RUBALE MWEMAGE A KIBONA IBWERA KATERERO MWEMAGE B KOBONA IBWERA KATERERO KANAZI KANAZI KATERERO KATERERO KATERERO KANAZI KATERERO KATERERO KARONGE KARONGE IBWERA KATERERO KAISHAZA KIBALE BUHENDANGABO BUGABO RUSHAKA B RUSHAKA BUHENDANGABO BUGABO KALEMA BUSHAGALA BUHENDANGABO BUGABO NYAKATO IGOMBE NYAKATO BUGABO KAAGYA MUSHOZI KAAGYA BUGABO

Lengo Kuu

Kuimarisha utawala bora (uwazi, uwajibikaji miongoni mwa watendaji kwa jamii, ushirikishaji wa wananchi katika kupanga, kutekeleza na kutathmini miradi ya maendeleo katika shule za msingi

Lengo mahususi

Zoezi hili la (PETS) lililenga kuishirikisha jamii katika mchakato wa kufuatilia mtiririko wa fedha za umma tangu zinapotolewa toka Serikali Kuu, kupitia ngazi za kati, yaani Halmashauri na Kata, hadi ngazi ya chini kwenye Kijiji ambako matumizi ya mwisho hufanyika katika kutekeleza miradi mbalimbali kama vile kujenga vyumba vya madarasa , zahanati, kisima cha maji, vifaa vya darasani kama vitabu, chaki na kadhalika. Lengo la PETS ni kuboresha na kuongeza ushirikishwaji wa jamii katika utekelezaji wa mipango tarajiwa na pia kufanya ufuatiliaji ili kuhakiki iwapo utekelezaji ulifanyika kwa uwazi na ufanisi.

Kufanyika kwa zoezi hili la PETS kuna uhusiano mkubwa na MKUKUTA (Mkakati wa Kupunguza Umaskini na Kukuza Uchumi Tanzania). Katika kutekeleza nguzo tatu za Mkukuta yaani Ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini wa kipato nguzo ambayo inaunganishwa na nguzo nyingine mbili za Kuimarisha ubora wa maisha na ustawi wa jamii na Utawala bora na uwajibikaji. Ni dhairi kuwa ushirikishwaji wa jamii kama mdau mmojawapo unasisitizwa katika kupanga, kutekeleza,kufuatilia na kutathmini shughuli mbalimbali za jamii ha hasa maendeleo ya Elimu ya Msingi. Ushiriki wa jamii katika mchakato huu pia ni muhimu kwa kuwa ni tafsiri mpango wa serikali wa kupeleka madaraka kwa umma kwa kukasimu mamlaka (D-by-D) ambapo mamlaka katika ngazi zote za Halmashauri ya Wilaya, Kata na vijiji yanaongezwa. Kwa hiyo pamoja na jamii kupitia kamati za Shule kushirikishwa katika mchakato wa kuainisha mahitaji na kuandaa mipango ya maendeleo katika shule zilizoko kwenye vijiji vyao, jamii inapaswa kupewa mlishonyuma na kufanya tathmini ili kujua kama kazi iliyofanyika inalingana na kiasi cha fedha kilichotumika( VALUE FOR MONEY).

Kwa mujibu wa Kifungu cha 3.1.1 cha mwongozo wa mujukumu ya Kamati za Shule module ya pili kilichochapishwa na Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inasisitizwa kuwa ili kusogeza madaraka karibu zaidi na wananchi mamlaka za ununuzi wa vifaa na mali kwa ajili ya shule umo mikononi mwa Kamati za shule na Halmashauri za vijiji na Kamati za Mitaa. Kwa mujibu wa mwongozo huo, Halmashauri za wilaya, Miji, Manispaa na Majiji watakuwa na jukumu la kutoa ushauri, utaalam, usimamizi na kushirikiana na Kamati za shule katika kutafuta vifaa na si vinginevyo.

Hatua hii inahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali na kuishirikisha jamii pana zaidi katika kufikia azma ya kuongeza kiwango cha uwazi na uwajibikaji kwa upande mmoja na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma zinazolengwa kwa upande mwingine.

Matokeo ya utafiti huu yanakusudiwa kuboresha na kuongeza ushirikishwaji wa wananchi/jamii katika kwa kwa kubainisha mianya ya ubadhilifu ili kuthibiti matumizi mabaya ya fedha za umma zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya elimu ya msingi.

Hii itawezesha

¨ Kusaidia kubaini ni wapi pakacha linavuja na kwa kiwango gani ili mianya hiyo izibwe.

¨ Kuimarisha utawala bora (uwazi, uwajibikaji miongoni mwa watendaji kwa jamii, ushirikishaji wa wananchi katika kupanga, kutekeleza na kutathmini miradi ya maendeleo katika shule za msingi

¨ Kutoa fursa kwa wadau kulinganisha iwapo kiasi cha fedha zilizotolewa zimetumika kama ilivyopangwa na kwa ufanisi wa kuridhisha.

¨ Kuhakiki iwapo matumizi ya fedha yanaonyesha au yanatoa picha ya thamani halisi ya fedha zilizotumika katika utekelezaji wa mradi husika.

¨ Ni mfumo wa kuiwezesha jamii kutambua mapungufu katika utendaji na kutoa mrejesho kwa watendaji kuhusu nini kifanyiwe maboresho katika maeneo yaliyobainishwa.

Njia za Uchunguzi (research methodology)

Mchunguzi alitumia njia mbalimbali za kupata taarifa kulingana na maudhui ya shughuli yenyewe ambazo zilihusisha kuongea na wadau wa sekta ya Elimu kama walimu wa shule za Msingi, wajumbe wa Kamati za Shule, Maafisa wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Vijijini, Wananchi wa kawaida, Wajumbe wa Kamati za TASAF na Wazabuni wakiwamo Watoaji wa Huduma mbalimbali zinazohusiana na Maendeleo ya Elimu ya msingi.

Njia zilizotumika kupata taarifa mbalimbali kwa sehemu kubwa zilihusisha mahojiano ya ana kwa ana na watoa taarifa (respondents) kwa kuwa ndio njia iliyoonyesha ufanisi zaidi katika kupata taarifa za kutosha. Hata hivyo njia nyingine kama kutomia madodoso maalum zilizotumika lakini kwa utaratibu wa mchunguzi kuuliza maswali ambayo yalikuwa kwenye madodoso hayo moja kwa moja na sio utaratibu uliozoeleka wa kusambaza madodoso kwa walengwa na kuwapa nafasi ya kujaza majibu kwa wakati wao.

Njia hii ya pili iliepukwa kwa vile ilionekana haitoi nafasi kwa mtafiti kuuliza maswali ya nyongeza kwa upande mmoja lakini inatoa mwanya kwa mtu aliyeulizwa kutoa majibu kwa nia ya kukwepa kutoa majibu yanayoweza kumuwajibisha.

Njia nyingine zilizotumika ni pamoja na kutembelea maeneo ya utafiti ili kujionea hali halisi (phsical observation) ikiwa ni pamoja na kutizama nyaraka mbalimbali (documentary review) kuthibitisha taarifa zilizotolewa wakati wa mahojiano. Jumla ya watu 144 walihusika katika kutoa taarifa zilizofanikisha utafiti huu.

Hata hivyo baadhi ya watu waliohojiwa walikubali kuhojiwa wakiwakatika maeneo ya wazi wakati wengine walipendelea kutoa taarifa kwa mtafiti faraghani.

Taarifa zilizokusanywa, ndio msingi wa kuandaa taarifa hii kwa kuonyesha matokeo ya utafiti, mapendekezo na changamoto zilizojitokeza wakati wa kufanya zoezi hili. Kufuatia matokeo yaliyopatikana wakati wa uchunguzi huu wa PETS, kuna haja ya kufanya shughuli ya aina hiyo katika maeneo mengine wilayani humo na mkoa wa Kagera kwa ujumla ili kuhusisha shule nyingi zaidi na kupata maoni ya wadau mbalimbali.

Matokeo ya Jumla:

· Uchunguzi umeonyesha kuwa jamii iko tayari kuchangia nguvu kazi katika maendeleo ya shule zao isipokuwa ukosefu wa uwazi katika kuwapatia taarifa mbalimbali jinsi michango yao inavyotumika unavunja ari ya wananchi kuchangia miradi husika.

· Imebainika kuwa shule nyingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijiji inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu pamoja na vifaa mbalimbali vya kufundishia kama vitabu. Mathalan, katika shule ya Maiga ambayo ina idadi ya wanafunzi 615(Darasa la Kwanza hadi la Saba) ukiongeza wanafunzi 50 wa darasa la awali, jumla ya wanafunzi katika shule hiyo ni 665. Kwa idadi hiyo shule hiyo ilitakiwa kuwa na vyumba 14 vya madarasa badala ya 9 vilivyopo. Upungufu huo wa vyumba vya madarasa unaifanya shule hiyo kuwa na wastani wa wanafunzi 73 wanaosomea katika chumba kimoja cha darasa hali inayoatrhiri ufundishaji. Idadi hiyo ya wanafunzi katika chumba kimoja cha darasa ni zaidi ya idadi inayotakiwa ya wanafunzi 45 kwa mujibu wa sera ya wizara.

· Ukosefu huo wa vyumba vya madarasa pia unazikabili shule nyingine za msingi ambazo ni pamoja na shule ya Mwemage A ambayo imelazimika kutumia jengo lililokuwa linatumika kama bwalo ili kupata vyumba viwili vya madarasa katika hali ya kukabiliana na upungufu huo. Shule hiyo ina vyumba vitano tu vya madarasa vinavyotumiwa na wanafunzi 315 na hivyo chumba kimoja kutumika kwa wanafunzi zaidi ya 60.

· Mfano mwingine wa upungufu wa vyumba vya madarasa ni katika shule ya Kanazi yenye wanafunzi 642 lakini ina vyumba sana tu vya madarasa idadi inayofanya wanafunzi zaidi ya 90 kusongamana katika chumba kimoja.

· Halikadhalika upungufu wa nyumba za walimu umejitokeza katika shule ya Mwemage A yenye upungufu wa nyumba sita za walimu na Karonge Shule ya Msingi inayopungukiwa nyumba 2.

· Wakati ni shule mbili tu za Mwemage B na Karonge miongoni mwa shule zilizotembelewa ndizo hazikuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa, ni karibu shule zote zilikuwa zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vitabu wa kati ya kitabu kimoja kutumika kwa wanafunzi wawili hadi 9. Shule hizo ni kama Maiga ambapo katika baadhi ya masomo kitabu kimoja hutumika kwa wanafunzi 9 hadi 40 badala ya sera ya angalau kitabu kimoja kutumiwa na wanafunzi wawili.

· Kwa mujibu wa matokeo ya ujumla ya utafiti huu, Shule ya Maiga pia ina upungufu mkubwa wa vyoo ambapo zaidi ya wanafunzi hutumia tundu moja la choo badala ya wanafunzi 20 hadi 25 kwa tundu moja kulingana na sera ya Taifa. Shule hiyo inatakiwa kuwa na matundu 24 ya vyoo badala ya 12 ya sasa.

· Ilibainika kuwa wajumbe wa Kamati za Shule hawatekelezi mujukumu yao ipasavyo si tu kutokana na baadhi yao kuwa na ufahamu duni wa mujukumu yao bali pia kutokuwa na njia za kipato ambapo baadhi yao hudiriki hushirikiana na watendaji wasiokuwa waadilifu kuhujumu maendeleo ya shule.

· Ilibainika kuwa baadhi ya Watendaji wa Halmashauri wanatoa maagizo yanayodhoofisha mamlaka ya Kamati za Shule katika kusimamia matumizi ya fedha na vifaa katika shule za msingi.

· Ilibainika kuwa walimu wakuu wa Shule za Msingi hawawashirikishi walimu wa kawaida katika kuainisha mahitaji ya shule kabla ya kukutana na wajumbe wa kamati ya shule kupanga matumizi ya fedha za capitation grant.

· Imebainika kuwa kutokana na ubadhilifu wa fedha baadhi ya shule zimekwama au zimetekeleza kwa kusuasua ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu chini ya Mpango wa Mendeleo ya Elimu ya Msingi MMEM.

· Imebainika kuwa fedha inayotolewa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu hazitoshelezi na matokeo yake shule hulazimika kujenga majengo yaliyochini ya viwango.

· Imebainika kuwa shule nyingi hazikaguliwi kwa wakati, hali inayotoa mwanya kwa walimu kutotekeleza mujukumu yao ikiwa ni pamoja na kusimamia matumizi ya fedha za umma na vifaa vya shule.

· Ilibainika kuwa shule nyingi zinatumia vitabu vya kumbukumbu za kihasibu baada ya matumizi ya fedha kwenye shughuli husika lakini kutokana na kukosa mafunzo ya kutosha matumizi ya vitabu hivyo huonekana kama mzigo mkubwa.

MATOKEO MAHSUSI

Imebainika kuwa shule mbili za Karama na Nsheshe ambazo ziko katika kijiji cha Nsheshe, Kata na tarafa ya Rubale zimeshindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu na vyumba vya madarasa kutokana na fedha iliyokuwa imetolewa kwa kazi hiyo kutumika vibaya.

Wakati shule ya msingi Karama ilikuwa imepanga kukamilisha ujenzi wa chumba kimoja cha darasa na nyumba moja ya mwalimu, Nsheshe ilikuwa imepanga kujenga nyumba moja ya mwalimu. Shule zote hizo ziko zaidi ya kilometa 80 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Bukoba vijijini. Taarifa zinasema kuwa kutokana na umbali huo shule hizo hazitembelewi mara kwa mara na viongozi wa halmashauri na hasa wakaguzi. Mwaka 2005 shule ya Karama ilipatiwa jumla ya shilingi ml 6.7 huku ml 3.1 zikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha Darasa na shilingi ml 3.6 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba moja ya mwalimu kazi ambayo haijakamilika miaka mitatu sasa.

Kukamilika kwa kazi hiyo ambayo pia ilitegemea mchango wa Nguvu za wananchi kungeifanya shule hiyo kuwa na upungufu wa chumba kimoja cha darasa kwa kuwa na jumla ya vyumba sita badala ya vitano vya sasa.

Halikadhalika ni walimu wawili tu wanaoishi katika nyumba ya walimu shuleni hapo na wengine 3 huishi zaidi ya kilometa 8 mbali na shule hiyo. Hali hiyo huchangia walimu kushindwa kutekeleza mujukumu yao ya kufundisha na kuathiri maendeleo ya taaluma shuleni hapo kutokana na kuchelewa kufika shuleni. Hali ya mahudhurio ya walimu wanaoishi mbali na eneo la shule huwa mbaya zaidi wakati wa majira ya mvua ambapo maeneo mengi ya njia zinazoelekea shuleni kutoka eneo la Nsheshe hujaa maji.

Kukwama kwa ujenzi wa shule hiyo kulitokana na shule hiyo kupoteza zaidi ya shilingi mil 3 ambazo zilikuwa zimepangwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi. Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa mwalimu huyo aliandika hundi ya malipo na kuikabidhi kwa kampuni moja ya Basinda Construction Company, ambayo haijatoa vifaa vilivyolipiwa hadi leo.

Hiki ni chumba cha darasa katika shule ya msingi Karama ambacho ujenzi wake ulikwama baada ya fedha za MMEM zilizokuwa zimetolewa kutumiwa vibaya na hivyo kutopatikana kwa vifaa kama mabati, misumari na mbao ili kukamalisha shughuli hiyo.Baadhi ya watoto wa shule hiyo wanasomea chini ya mwembe baada ya kukosa mahali pa kusomea.

Hadi ujenzi wa nyumba ya mwalimu unakwama ulikuwa umefikia hatua ya linta wakati ule wa chumba cha darasa ulikuwa umefikia hatua ya kuezeka. Ni baada ya shinikizo kutoka kwa Kamati ya shule kwa uongozi wa halmashauri ya Wilaya, ndipo, mhusika mkuu( aliyekuwa mwalimu Mkuu wa shule hiyo) alipogharimia vifaa mbalimbali kwa fedha yake na kulifikisha jengo hilo hadi hatua ya kuezekwa na zaidi ya miaka 2 sasa hakuna kinachofanyika.

Kutokana na kutelekezwa, vichaka vimeota ndani ya jengo hilo ambalo sambamba na chumba kimoja cha darasa kisichokamilika kutokana na matumizi mabaya ya fedha vinaonekana kama magofu katikati ya majengo mengine yaliyo katika eneo hilo.

Wakati ujenzi wa nyumba ya mwalimu ulikwama katika hatua ya hanamu, tayari chumba cha darasa kilishawekewa papi lakini mabati na misumali ndivyo havikupatikana baada ya ubadhilifu huo unajitokeza.

Matokeo yake tayari mbao zilizowekwa juu ya chumba cha darasa kwa ajili ya shughuli za kuezeka zimeanza kupinda sambamba na zile zilizotayarishwa kwa ajili ya nyumba ya walimu. Katika hali hiyo itabidi zinunuliwe mbao nnyingine na zifungwe upya endapo fedha ya mabati itapatikana na shughuli ya kuezeka majengo hayo kufanyika.

Nalo jengo la nyumba ya walimu katika shule ya Msingi Nsheshe lilikwama wakati limefikia hatua ya kuezekwa.

Picha hii hapo juu inaonesha nyumba ya walimu katika shule ya msingi Nsheshe ambayo ujenzi wake ulikwama kutokana na ubadhilifu wa fedha.Kama nyumba hiyo ingekamilika ingeondoa tatizo la walimu kuishi mbali na shule na hivyo kuchelewa kufika shuleni hivyo kuathiri ufundishaji.

Taarifa zilizopatikana zinadai maafisa fulani wa halmashauri waliwaagiza walimu wakuu wa shule hizo waandike hundi za malipo kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi katika duka lililomilikiwa na Lugaiyamu Basinda ambaye hakutoa vifaa baada ya kupokea malipo hayo. Ingawa hakuna maandishi yanayoonyesha madai ya walimu hao kuelekezwa hivyo kukiukwa kwa taratibu za manunuzi kunajenga mazingira yanayoonyesha maafisa wa Halmashauri kuhusika na upotevu huo.

Kulingana na miongozo iliyopo, masuala yanayohusiana na manunuzi ya vifaa vya shule hujadiliwa na Kamati za Shule husika baada ya kuainisha mahitaji. Baada ya hatua hiyo, mtunza stoo hutembeza karatasi maalum ya kulinganisha bei (quotation) kwa wenye maduka ya vifaa vinavyohitajika. Baada ya hapo ndipo kamati hukubaliana juu ya mtu atakayetoa vifaa hivyo kwa kuangalia mwenye bei nafuu na kisha mwalimu huandika hundi ya malipo baada ya kupokea vifaa hivyo.

Hata hivyo, Mhandisi wa Halmashauri ambaye anatakiwa aione orodha ya vifaa vilivyonunuliwa na kudhibitisha kama vimepelekwa eneo husika hakufanya hivyo kabla ya kuidhinishwa kwa malipo ya vifaa. Katika hili maafisa wa halmashauri wanaohusika na utaratibu wa kuidhinisha malipo pamoja na mwalimu mkuu wa shule zinazodai kutapeliwa vifaa vya ujenzi wanawajibika kwa hasara iliyosababishwa kwa kuwa hawakutekeleza wajibu wao kama taratibu zinavyopaswa.

Viwango hafifu vya majengo ya shule nyingi za msingi katika wilaya ya Bukoba vijijini vinaweza kufanya majengo hayo kuanza kuharibika baada ya muda mfupi kama inavyoonesha kwenye chumba hiki katika shule ya msingi Karama ambacho madirisha yake tayari yameanza kuharibika.Pamoja na picha hiyo ni mbao ambazo zimeanza kupinda baada ya kukaa zaidi ya miaka miwili bila kutumiwa katika ujenzi wa jengo lililokwama.

Wajumbe wa Kamati ya Shule ya Karama wanadai ni hadi waliposhindwa kuona maendeleo ya ujenzi wa shule ndipo walipoandamana hadi ofisi ya serikali ya kijiji ili kupata maelezo na ndipo Mwalimu Mkuu alipotoa taarifa ya kutapeliwa.

Hata hivyo baadhi ya nyaraka mbalimbali na taarifa zilizopatikana wakati wa zoezi hili, zinaonyesha Viongozi wa Idara ya Elimu wamekuwa wakitoa maagizo mbalimbali ambayo yanadhoofisha uwezo na uhuru wa Kamati za Shule katika kutekeleza mujukumu yake. Upo ushahidi wa madai kuwa Walimu wa shule zilizotapeliwa vifaa vya ujenzi waliagizwa kununua vifaa katika Duka la Basinda na kuagizwa kuidhinisha malipo hata kabla ya kupokea vifaa kama taratibu zinavyoagiza.

Malalamiko hayo ya walimu waliotapeliwa kuwa walilazimishwa ama kuelekezwa kununua vifaa vya ujenzi kutoka kwa mfanyabiashara huyo hayana ushahidi wa maandishi. Hata hivyo kutokana na idadi kubwa ya shule zilizonunua vifaa kutoka kwa mfanyabiashara huyo hata zile ambazo hazikutapeliwa, upo ushahidi wa kimazingira kuwa shule hizo hazikununua vifaa huko kwa bahati mbaya (coincidence) bali kwa kuelekezwa. Hii inatokana na ukweli kuwa jambo hili lilijitokeza katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi na sio katika ununuzi wa vifaa vingine vya shule kama vifaa vya kufundishia ikiwamo vitabu ambapo aghalabu shule zimenunua vifaa hivyo kutoka kwa wafanyabiashara tofautitofauti.

Hata hivyo upo ushahidi kimaandishi kuwa wakati fulani viongozi wa Idara ya Elimu katika Halmashauri hiyo wamewahi kutoa maagizo ambayo yanaashiria kukandamiza mamlaka ya kamati za shule na hata kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma.

Mnamo tarehe 13, Mei 2008, Afisa Elimu wa halmashauri ya Wilaya ya Bukoba aliawaandikia walimu wakuu wote wa shule za msingi wilayani humo akiwaagiza kutumia sehemu ya fedha inayotolewa kwa utaratibu wa Capitation Grant kinyume na mwongozo wa matumizi ya fedha hizo.

Barua hiyo yenye kichwa cha habari: KUGHARIMIA SCANNING YA TSM9 ZA WANAFUNZI WA DARASA LA VII na Kumb Na. BDC/E/E.5/3/VOL.6/69, inawaagiza walimu wakuu kutumia fungu la mtihani kwenye fedha ya capitation kulipia gharama za kuscan fomu zenye picha za wanafunzi wa darasa la saba kwa ajili ya mtihani wa kitaifa.

Hata hivyo, barua hiyo pia inawaelekeza shughuli hiyo ifanywe na kampuni ya Benny Bazaar kwamba ni mwenye gharama nafuu dhidi ya wengine, hata bila kuainisha ni utaratibu gani umefuatwa kulinganisha bei kwa mujibu.

Sehemu ya barua hiyo inasomeka “……………kwa kuwa shughuli hii ni nyeti, inaagizwa zoezi hili lifanywe na Kampuni moja. Kwa kuwa Benny Bazaar ina bei nafuu dhidi ya kampuni nyingine ndiye ahusike.

Barua hiyo iliyosainiwa na H. Batinoluho, inaendelea kuagiza……

………………….taratibu zote za malipo zifuatwe na mzabuni awe amelipwa kabla ya Mei 31, 2008.

Maagizo haya ni kinyume na mwongozo wa matumizi ya fedha za umma zinazopelekwa katika shule za msingi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya elimu kwa kuwa yanawapokonya wajumbe wa kamati za shule uhuru wa kuainisha mahitaji yao na kupendekeza huduma inayotakiwa kutolewa na mtu mwenye huduma yenye ubora na gharama nafuu.

Taarifa inaonesha kuwa maagizo ya aina hiyo yamekuwa yakitolewa kwa kipindi cha miaka miwili hivi iliyopita na walimu wa shule nyingi za msingi wamelazimika kuchukua fedha kutoka mafungu mengine ya Captation grant baada ya kuwa na fedha pungufu kwenye fungu la mtihani. Halikadhalika kutokana na mwongozo wa matumizi ya fedha kwenye miradi ya maendeleo ya elimu ya msingi kupitia utaratibu wa capitation, fungu la mtihani ambalo ni aslimia 10% ni kwa ajili ya shughuli zote za mitihani katika shule husika.

Kutokana na kutumia fedha hizo kwa shinikizo kutoka Halmashauri karibia shule zote zimelazimika kutoa fedha katika maeneo mengine kama ukarabati, utawala na kadhalika na hivyo shughuli katika maeneo husika kukwama ikiwa ni pamoja na baadhi ya shule kushindwa kugharimia mitihani kwa madarasa yaliyobaki jambo linaloathiri maendeleo ya mtihani kwa kiwango kikubwa.

Mathalan wakati agizo hilo linatolewa, Shule ya Msingi Mwemage A ilikuwa na shilingi 12,874.40/= katika fungu la mitihani na kwa vile fedha hiyo ilihitajika ilipwe ndio watoto waweze kufanya mitihani, shule hiyo ililazimika kuchukua kiasi cha shilingi 82,676/= kwenye fungu la ukarabati ili kugharimia scanning ya picha kwa ajili ya watahiniwa 49 wa darasa la saba kwa gharama ya shilingi 1950/= kwa kila fomu ya TSM9 yenye picha.

Shule hiyo ambayo kabla ya kumilikiwa na Serikali mwaka 1970, ilianzishwa na Kanisa la Kikatoliki mwaka 1960 na inahitaji ukarabati mkubwa ikiwa ni pamoja na kuezeka upya majengo yake. Kwa sasa majengo ya shule hiyo yameezekwa kwa mabati aina ya asbestos ambayo yameharibika vibaya na wanafunzi hunyeshewa darasani wakati wa mvua.

Ukichukua takwimu za watahiniwa 8548 waliofanya mtihani wa Darasa la saba mwaka huu katika wilaya ya Bukoba vijijini kwa kuzidisha na gharama ya kuscan fomu ya TSM9 moja ni sawa na 16,668,600= ambazo kampuni ya Benny Bazaar imelipwa bila hata utaratibu wa kushindanisha au kutangaza zabuni kwa mujibu wa taratibu. Taarifa zinaonyesha kuwa utaratibu wa kuwashurutisha walimu wakuu kugharimia scanning umekuwa ukifanyika kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo ilipoanza kuscan form za TSM9 baada ya utaratibu wa zamani ambapo picha zilikuwa zinabandikwa kwenye form kuwa na matatizo ya watahiniwa kupoteza picha zao baada ya kubanduka kwenye form. Kwa hali hii wastani wa milioni 50,005,800= za capitation grant zinaweza kuwa zimetumika katika kipindi cha miaka mitatu tangu utaratibu huo wa kuzishurutisha kamati za shule ulipoanza.

Barua hiyo haikuwa ya kwanza kuandikwa kwa walimu wakuu ili kuwapatia maelezo ya namna ya kutumia fedha za shule au kuwachagulia mtu, Kampuni ya kuwasambazia bidhaa wanazozihitaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya shule.

Barua ya Decemba 22, 2004 iliyosainiwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba vijijini inaitambulisha kwa walimu wakuu wote wa wilaya hiyo kuwa Kampuni ya Alpex imeruhusiwa kuendesha shughuli za uuzaji vitabu na vifaa vingine vya kielimu katika halmashauri hiyo. Kwa mujibu wa mwongozo wa usimamizi wa fedha na vifaa vya shule Kamati za Shule ndizo zenye mamlaka ya kupendekeza/kuchagua mzabuni wa kuwapatia huduma wanayohitaji baada ya kufuata taratibu zote za manunuzi na sio Viongozi wa Halmashauri kuelekeza au kupendekeza mtu au kampuni inayostahili kutoa huduma hiyo.

Kimantiki sio jambo la ajabu kwa uongozi wa halmashauri hiyo kufanya utambulisho wa Kampuni zinazohitaji kupata soko la kuuza bidhaa mbalimbali kwa shule za msingi. Jambo la kushangaza kuhusu utaratibu huu ni pale ambapo utambulisho wa aina hiyo hufanywa kwa kambuni fulani pekee na wakati mwingine viongozi wa halmashauri ya wilaya kudaiwa kuwaelekeza au kuwashurutisha walimu wakuu kufanya bishara na Kampuni fulani na kuwazuia wasinunue bidhaa kutoka kwa maduka fulani ambayo kamati za Shule ziumeamua zenyewe kwa kufuata mwongozo wa matumizi ya fedha za maendeleo ya elimu ya Msingi.

Walimu waliohojiwa wanakiri kuwa pamoja na kuwa matumizi hayo ni kinyume na utaratibu uliopo, yapo maneno katika barua yenye agizo hilo ambayo yanawafanya walimu wasiwe na pingamizi lolote kutekeleza maamuzi hayo ya wakuu wao wa kazi. Mfano barua hiyo inatoa nakara kwa waratibu elimu wa kila kata kuwaagiza wahakikishe agizo hilo linatekelezwa, hali inayofanya kuchagua kuheshimu matakwa ya wakubwa wao wa kazi na kudharau muongozo wa matumizi ya fedha za shule.

Inaagizwa katika moduli ya pili ya mwongozo wa uimarishaji wa uwezo wa wajumbe wa Kamati za Shule za Msingi juu ya Mpango shirikishi, usimamizi wa fedha na vifaa Kifungu cha 3.1.2 ( Taratibu za Kumpata Mzabuni kwa Ununuzi wa Vifaa/Bidhaa/ Huduma ukurasa wa 43 kuwa:

“Utaratibu wa ununuzi wa vifaa vya shule unaokubalika na Serikali ni ule wa kutumia mzabuni. Mzabuni ni mtu binafsi, kikundi cha watu, au kampuni ambayo imeandikishwa kisheria kuuza bidhaa au vifaa na awe ameingia mkataba baina yake na shule. Muuzaji huyo awe na namba ya utambulisho kama mlipa kodi. Uchaguzi wa mzabuni wa shule utafanywa na Kamati ya Shule baada ya kuchambua sifa za vifaa na huduma inayotakiwa kutoka kwa wazabuni mbalimbali.”

Katika hili utafiti huu umebaini kuwa kama ungefanyika utaratibu wa kuwashindanisha wazabuni mbalimbali, gharama za kuscan za watahiniwa wa mtihani wa Darasa la Saba TCM9 katika ya maduka kama Church Bookshop, New Bukoba Cyber Centre, na Morden Secretarial Services zote za mjini Bukoba, gharama za kuscan form moja zingekuwa kati ya shilingi 500 hadi 1000 badala ya 1950 alizolipwa Benny Bazaar.

Hili ndilo jengo la nyumba ya walimu katika shule ya Msingi Karama ambalo lilikwama kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha za MMEM

Agizo lingine ni lile lililokuwa linawaelekeza walimu hao kutumia fedha za Captation kugharimia mafunzo ya walimu ambao walitakiwa kwenda kuhudhuria mafunzo kuhusiana na maboresho ya mtaala.

Hali hii inawafanya walimu na wajumbe wa kamati za shule Kwa ujumla kuamini kuwa katika halmashauri kuna mawakala wa watu wanaopendekezwa kupewa kazi ya kutoa huduma mbalimbali ikiwamo ununuzi wa vifaa.

Kutokana na hitilafu hii walimu wa shule zilizopoteza fedha wakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu wamedai kuwa wamekuwa wakielekezwa maduka ya kununua vifaa mbalimbali vya shule na hundi za walimu wanaokaidi maagizo hayo hucheleweshwa kuidhinishwa ama kukataliwa.

Kuna taarifa kuwa hivi karibuni baadhi ya walimu wameelekezwa kufanya manunuzi ya vitabu kwenye Kampuni binafsi iliyoko mjini Bukoba, tofauti na Kampuni ya MBESA BOOKS DISTRIBUTORS LTD kwa madai kuwa gharama za vitabu za Kampuni hiyo ni za juu. Baadhi ya shule hizo ni Kamuli, Butainamwa, Nsheshe na Kobunshwi ambazo zinadaiwa malimbikizo ya gharama za ununuzi wa vitabu kutoka Kampuni ya Mbesa. Kampuni hii ilipata umaarufu wakati wa mradi wa kusambaza Tusome Vitabu wa CARE, mradi uliofanikiwa sana katika maeneo mengi ya wilaya hiyo na Shule nyingi zinatumia huduma zake.

Mbali na shule za Nsheshe na Karama zilzizofuja fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu kama ilivyoelezwa hapo juu, taarifa zilizopatikana wakati wa uchunguzi huu, zinataja baadhi ya shule nyingine za Buzi (tarafa ya Bugabo),Nyakabulala(Rubale),Butulage(Rubale) na Umoja(Rubale).

Baadhi ya shule, mfano Shule ya Msingi Katerero zilipoteza fedha za ununuzi wa mbao ambapo kampuni ilipewa zabuni ya kuwapatia mbao za Pine, lakini badala yake zikatolewa Griveria ambazo sasa zimebunguliwa mbali na wahusika kuhalalisha malipo kwa bidhaa hiyo.

Shule hizo zinadaiwa kupoteza fedha kwa kampuni ya vifaa vya ujenzi ambayo ilipokea malipo lakini ikashindwa kutoa vifaa hali iliyosababisha majengo yaliyotarajiwa kujengwa kwa fedha hiyo kukwama au kuendelea kwa kusuasua baada ya walimu waliohusika kushinikizwa kutoa fedha yao kuyakamilisha.

VIWANGO VYA MAJENGO/VIFAA (Value for Money)

Taarifa nyingi zilizopatikana wakati wa uchunguzi huu zinaonesha kuwa majengo mengi iwe ni vyumba vya madarasa au nyumba za walimu yako chini ya viwango. Hii inatokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na udhibiti mdogo wa vifaa vinavyonunuliwa kwa ajili ya majengo hayo na utaalam duni unaotumika katika ujenzi ambao ni pamoja kutumia vipimo hafifu hasa wakati wa uchanganyaji wa saruji ili kukamilisha jengo husika kwa fedha kidogo iliyotengwa.

Mathalan, fedha inayotolewa kwa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa kupitia mpango wa Maendeleo ya elimu ya Msingi(MMEM) ni shilingi ml 3.1, wakati ikiwa jengo kama hilo lingekuwa linajengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF), zaidi za shilingi milioni kumi zingehitajika.

Shilingi milioni 3.1 kwa ujenzi wa chumba kimoja cha darasa na shilingi milioni 3.6 kwa nyumba ya mwalimu ni viwango ambavyo vimekuwapo tangu mwaka 2001 wakati miradi ya MMEM ilipoanza lakini bei ya bidhaa mbalimbali za ujenzi imekuwa ikipanda kila kukicha.

Lakini la kushangaza ni taarifa za baadhi ya wajumbe wa Kamati za Shule kuhusika na wizi wa vifaa vya ujenzi. Hii inatokana na wengi wa wajumbe wa Kamati za Shule kuwa na kipato duni au kutokuwa na kipato kabisa lakini wanapewa kazi ya kusimamia Utendaji wa watu wanaolipwa ujira kama mafundi Ujenzi na Walimu wakuu wakati wa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya shule.

Huu ni Msingi wa jengo la chumba cha Darasa katika shule ya Msingi Karama ambalo pia halikukamilia kwa madai ya ubadhilifu.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati waliohojiwa, walikiri ama kuona au kushiriki katika wizi wa saruji kwa kushirikiana na mafundi ili kupata fedha za kujikimu. Wajumbe wa Kamati za shule katika maeneo yaliyotembelewa ni watu wanaojiajiri (wenye kipato duni), na hukabidhiwa jukumu la kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo wakati hawana namna yoyote ya kujikimu. Wakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa wajumbe wa kamati hupangiwa zamu kwa muda wa wiki mojamoja ili kuhakikisha udhibiti wa vifaa.

Kuna Taarifa kuwa kutokana na Wajumbe wa Kamati za Shule ama kukosa umakini katika kutekeleza mujukumu yao au kwa kupatiwa fedha kidogo ya kujikimu hula njama na baadhi ya walimu wakuu wa shule kughushi sahihi za mihutasari ya vikao vya kamati ili kufanya manunuzi hewa hasa kwa kutumia fedha ya Capitation ambayo hutolewa kwa ajili ya maendeleo ya shule kwa uwiano wa idadi ya wanafunzi wa shule husika.

CHANGAMOTO

Zipo changamoto nyingi ambazo zinatoa mwanya wa matumizi mabaya ya fedha au kukwamisha maendeleo ya elimu ya msingi kwa ujumla katika wilaya ya Bukoba vijijini kama ifuatavyo:

· Changamoto ya kwanza ni la Kimfumo zaidi ambapo Utendaji Kazi wa walimu wakuu wa shule nyingi za msingi ambao kimsingi wanawajibika kwa Kamati za Shule katika mambo ya kiuendeshaji, hujikuta wakilazimika kuwajibika zaidi kwa wakuu wao wa kazi(Afisa Elimu, au baadhi ya maafisa waandamizi wa Idara hiyo) hata katika kutimiza maagizo ambayo yanakinzana na Maagizo ya Kamati za Shule. Walimu hufanya hivyo kwa kuhofia kupoteza ajira zao au kupata adhabu kutokana na kukaidi maagizo ya wakuu wao wa kazi na kuheshimu matakwa ya Kamati za Shule.

· Shule nyingi za msingi ambazo ziko umbali wa zaidi ya kilometa 80 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Vijijini kama Nsheshe na Karama kutembelewa mara chache sana katika kipindi kirefu na wakaguzi wa Halmashauri hiyo. Hali hiyo inaathiri utendaji wa walimu wa shule hizo kama ilivyodhihirika kwa shule hizo ambazo huchukua kipindi cha takriban miaka mitatu hadi mitano kutembelewa na maafisa wa idara hiyo.

Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa hata wakati wa ujenzi wa majengo yaliyokwama katika shule ya msingi Karama, Mhandisi wa Halmashauri hakuwahi kufika kukagua hatua mbalimbali za ujenzi kama taratiubu zinavyotakiwa hadi wakaguzi wa ndani walipofika baada ya ujenzi kukwama.

· Hata hivyo si kila tatizo linalotokea katika usimamizi mbovu wa matumizi ya fedha au miradi mbalimbali ya maendeleo ya shule za msingi zilizotembelewa unatokana na utendaji mbovu wa maafisa wa halmashauri au wajumbe wa Kamati za shule.

Halmashauri ya wilaya ya Bukoba inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa fedha za kuendesha shughuli za ukaguzi wa mara kwa mara hasa katika miradi inayofanyika kwenye maeneo yaliyoko mbali na makao makuu ya halmashauri hiyo. Baadhi ya maafisa wa idara ya ukaguzi waliohojiwa walisema kuwa shughuli za ukaguzi wa shule hazijafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu sasa.

· Tatizo jingine ni kwamba walimu wanaosimamia maazimio ya Kamati za Shule pamoja na Wajumbe wa Kamati hizo wenyewe hawana elimu ya kutosha kuhusu majukumu yao. Kabla ya kuanza kwa mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi, wajumbe wa Kamati hizo walipewa mafunzo lakini yalikuwa ya muda mfupi kiasi kwamba wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kama mwongozo unavyoelekeza.

· Karibia aslimia 90 ya wajumbe wa Kamati za Shule waliohojiwa wakati wa utafiti huu, walipendelea usimamizi wa shughuli za Kamati za Shule zibakie mikononi mwa wajumbe wasiokuwa walimu na walimu waendelee na majukumu yao ya kufundisha wakati ni chini ya aslimia 10 walioona vyema walimu waendelee kutekeleza majukumu ya kamati hizo kama ilivyo sasa. Hii inatokana na taarifa zilizopatikana kwa kutumia madodoso.Katika swali namba 9 (a) na (b) wajumbe wa Kamati za Shule walitakiwa kutoa maoni ikiwa ni vyema walimu ambao majukumu yao ya kimsingi ni kufundisha waendelee kuwamo katika Kamati za Shule ili hali muda wao wa kuwa darasani unapungua kwa sababu ya shulghuli za Kamati. Swali hili ambalo pia lilikuwa linatoa nafasi ya kupendekeza nini kifanyike ili kufidia vipindi vinavyopotea kutokana na walimu kuwa katika shughuli za Kamati, ni miongoni mwa maswali yaliyolenga kupata maoni kama wajumbe wa Kamati za Shule wanaotokana na jamii wanashiriki kikamilifu katika kudhibiti na kusimamia matumizi ya fedha za umma badala ya kazi hiyo kuachiwa walimu kama ilivyobainika.

· Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Shule wasiokuwa walimu walionekana kutokuwa na taarifa muhimu za maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika shule zao na kusisitiza kila wakati kuwa mwenye taarifa fulani, mfano idadi ya mifuko ya saruji iliyotumika katika ujenzi wa jengo fulani ni Mwalimu Mkuu au Mtunza stoo. Hali hii ilijitokeza wakati wajumbe wa kamati za Ujenzi ndio waliuokuwa wanapaswa kusimamia vifaa vya ujenzi wakati miradi husika inaendelea.

· Wajumbe waliohojiwa walipendelekeza wapewe mafunzo zaidi ya usimamizi wa Uendeshaji wa shughuli za Kamati.

· Pia imebainika kuwa fedha inayotolewa kwa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa haitoshelezi mahitaji na badala yake miradi hiyo hutekelezwa chini ya viwango au kususua na hasa kutokana na kwamba ari ya wananchi kuchangia maendeleo yake ni ndogo kutokana na kwamba mara nyingi miradi hiyo hupangwa kutoka juu na sio chini.

· Watu waliohojiwa walishauri kuwa badala ya kutenga shilingi 3.1 za ujenzi wa chumba cha darasa na shilingi ml 3.6 za nyumba ya mwalimu ambazo hazitoshi kufanya kazi hiyo, ingekuwa vema zaidi fedha hiyo ikatumika kukarabati vyumba vilivyoko katika hali mbaya au kujenga mojawapo ya majengo hayo badala ya kujenga majengo yote na kushindwa kuyakamilisha kwa wakati mmoja kutokana na uhaba wa fedha.

· Hata hivyo ilibainika kuwa miradi yote ya ujenzi iliyotekelezwa chini ya TASAF au World Vision ilikamilika kwa viwango na kwa muda uliopangwa si kutokana na usimamizi wake tu bali na kwamba huibuliwa na wananchi nap engine kupigiwa kura kutokana na umuhimu wa mradi husika na hivyo ari ya wananchi kuchangia maendeleo yake huwa ni ya kiwango kikubwa. Kwa hiyo katika maeneo mengi yaliyotembelewa na hata wiyala ya Bukoba vijijini kwa ujumla imeonekana kuwa wananchi wa maeneo hayo wana ari ndogo ya kuchangia miradi hiyo kwa kuwa wanaona kwa mfano si kipaumbele kujenga chumba kipya cha darasa au nyumba ya mwalimu wakati wanafunzi hawana madawati ya kutosha na nakadhalika.

Hii ni picha ya choo inayotumiwa na familia inayoishi katika nyumba ambamo Mwalimu Alfred Jeremiah anapanga.Kama wananchi wangeshirikishwa katika kuamua miradi ipi ipewe kipaumbele katika maendeleo ya elimu ya msingi basi ingepanga kutekeleza miradi kwa lengo la kuwaondolea walimu adha kama inayompata mwalimu huyu.

MALIWATO (bafu)

Hii nayo ni picha ya Bafu inayotumiwa na familia inayoishi katika nyumba ambamo Mwalimu Alfred Jeremiah anapanga.Kama wananchi wangeshirikishwa katika kuamua miradi ipi ipewe kipaumbele katika maendeleo ya elimu ya msingi basi ingepanga kutekeleza miradi kwa lengo la kuwaondolea walimu adha kama inayompata mwalimu huyu.

· Kutokana na hali iliyoelezwa hapo juu baadhi ya shule kwa mfano, zinapangiwa kujenga nyumba za walimu wakati nyumba zilizoko hazina walimu wanaoishi humo. Baadhi ya shule hizo ni kama Nyakato ambako kuna nyumba moja isiyokuwa na walimu wanaoishi. Kwa mfano zipo taarifa kuwa moja kati ya nyumba 2 za walimu katika shule ya Msingi shule Kitunga iliyoko Kata ya Butelankuzi inakaliwa na Mwalimu wa Sekondari na nyingine Afisa Mtendaji wa Kijiji baada ya kukaa bila walimu wanaoishi shuleni hapo. Jambo hili la walimu kutopendelea kuishi katika nyumba za walimu zilizojengwa maeneo ya shule ni moja ya sababu ya wananchi wengi wilaya ya Bukoba vijijini kuwa na ari ndogo ya kuchangia ujenzi wa nyumba hizo ambazo matokeo yake hazitumiki.

· Halikadhalika ilibainika kuwa kwa kuwa miradi ya ujenzi inayotekelezwa kwenye shule husika huchukuliwa na baadhi ya wanasiasa kama sera na kipimo cha kujinadi wakati wa kuomba kura kwenye uchaguzi unaofuata, hakuna kiongozi yeyote anayeweza kukubali mapendekezo ya kutumia fedha za ujenzi wa chumba cha darasa au nyumba ya mwalimu kwa kazi tofauti hata kama kwa kufanya hivyo kuna lenga matumizi yenye tija.

· Baadhi ya watu walio na uhusiano na miradi iliyokuwa ikitekelezwa chini ya mpango wa World Vision wanasema kuwa hata malipo kwa watu wanaotoa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya miradi yake hutakiwa kutoa vifaa vilivyoagizwa kwa kuandikiwa LPO na malipo hufanyika baada ya vifaa kufikishwa kwa mnunuzi tofauti na ilivyojitokeza kwenye shule zilizotapeliwa.

· Hata hivyo wanashangaa kwa kuwa Shule za Msingi ni taasisi za Serikali na haiwezekani mfanyabiashara yeyote akatapeli vifaa vya shule halafu asichukuliwe hatua za kisheria!

· Miradi yote ya World Vison iliyotekelezwa katika shule za Mwemage B, Maiga, Kaishaza B na Kalema ni mfano wa kuigwa na miradi mingine katika kusukuma maendeleo ya shule.Hii inajidhihirisha hata katika mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ambayo ilikamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

· Karibia asilimia 90 ya shule za msingi katika maeneo yaliyotembewa zimekuwa na kiwango kikubwa cha wanafunzi wanaofaulu kwenda shule za sekondari. Hata hivyo hali hiyo haimaanishi kuongezeka kwa kiwango cha elimu. Hii inatokana na ukweli kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hushinda kwa alama za chini na kusajiliwa katika shule za sekondari za kata ambazo nyingi zake hazina vifaa vya kufundishia sambamba na walimu.

· Maeneo mengi ya vijijini hayana maduka ya kuuza vifaa vinavyotakiwa na hata wakiwa navyo wengi wao hawawezi kutoa nyaraka mbalimbali zinazohitajika kisheria kwa ajili ya kumbukumbu za kihasibu. Mathalani kuna wafanyabiashara wawili tu wanaouza vifaa vya ujenzi katika kata ya Rubale zilipo shule za Karama na Nsheshe. Ni maduka haya tu ambayo yanaweza kutumika kutoa vifaa vya ujenzi na kutoa stakabadhi muhimu zinazohitajika endapo shule hizo zingeamua kuchukua vifaa vya ujenzi katika eneo hilo badala ya kulazimika kununua vifaa Mjini Bukoba kutokana na maduka mengi ya vijiji kutokuwa na bidhaa za kutosha au kutokuwa na nyaraka muhimu ikiwamo stakabadhi zinazohitajika kwa ajili taratibu za kihasibu.

MAPENDEKEZO:

· Baada ya changamoto zilizoainishwa, taarifa zilizopatikana zinaashiria mapendekezo yafuatayo:

· Kuna haja ya kuwa na mafunzo zaidi kwa wajumbe wa Kamati za Shule ili kufanikisha utekelezaji wa Majukumu yao ambayo ni pamoja na usimamizi thabiti wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya elimu ya Msingi.

· Kuna haja ya kutenga fedha zaidi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu badala ya viwango vya zamani vya shilingi 3.1ml na ml 3.6 ili kuhakikisha majengo yanakamilika katika muda uliopangwa na kwa viwango vya kuridhisha. Viwango hivyo vilipangwa tangu mwaka 2000 wakati wa kuanza kwa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) kabla bei za bidhaa mbalimbali kupanda kama ilivyo sasa. Miradi inayoibuliwa chini ya Mpango wa TASAF au kutekelezwa na mashirika mengine kama World Vision mathalan hupangiwa fedha ya kutosha kwa kuwa makadirio ya bajeti hufanyika kwa kuzingatia mazingira na bei za wakati husika.

· Kuna haja ya kupambanua majukumu ya Kamati za Shule na yale ya Halmashauri kiutendaji katika kufanya maamuzi ya namna ya kutumia fedha za maendeleo ya Elimu ya Msingi ili kuepuka matumizi yasiyoendana na mwongozo wa Usimamizi wa Fedha na Vifaa vya Shule.

· Uongozi wa Halmashauri unapaswa kuchunguza tuhuma za upotevu wa vifaa vya ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu katika shule za Karama, Nsheshe na nyinginezo na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi mabaya ya fedha za Umma.

· Ni Muhimu walimu wakuu wa shule za Msingi pamoja na viongozi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa wanafuata miongozo katika kutumia fedha zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya Elimu ya Msingi.

· Kuna haja ya kufanya upya tathimini ya mahitaji ya vyumba vya madarasa na nyumba za walimu katika shule mbalimbali za msingi kwenye wilaya ya Bukoba Vijijini ili kubaini ni wapi pa kupewa kipaumbele tofauti na hali ya sasa ambapo mgawanyo wa fedha kwa ajili ya shughuli hiyo hufanyika kwa matakwa ya kisiasa. Kutokana na mgawanyo wa fedha kwa ajili ya miradi ya elimu kufanyika kwa matakwa ya kisiasa, shule kama Mwemage A iliyokuwa chini ya uangalizi wa Kanisa la Kikatoliki kabla ya kumilikiwa na serikali haijawahi kupata fedha za ujenzi tangu kuanza kwa MMEM mwaka 2000 wakati wanafunzi wa shule hiyo wanatumia jengo lililokuwa linatumika kama bwalo la chakula kama darasa. Kuna taarifa kuwa tathimini ya hali ya vyumba vya madarasa na nyumba za walimu iliyofanywa na DANIDA kabla ya kuanza kwa utelekezaji wa MMEM haikubainisha mahitaji halisi ya majengo yao.

Hili ni jiko katika shule ya Msingi Maiga lakini tofauti na miradi ya TASAF,miradi mingi ya ujenzi katika shule za msingi hutekelezwa kwa shinikizo la wanasiasa na siyo maamuzi ya wananchi wenyewe.Kama wangeshirikishwa wananchi wanaosishi karibu na shule ya Msingi Maiga pengine wangeamua kujenga jiko hili linalotumiwa na walimu kama kipaumbele chao.

· Ni vyema uwepo mpango utakaohakikisha kuwa walimu ambao majukumu yao ya kimsingi ni kufundisha wanapewa nafasi ya kutimiza wajibu wao huo kwa kuwapa uwezo zaidi Wajumbe wa Kamati za Shule kuhusika badala ya majukumu yote kuachiwa walimu kama ilivyo sasa. Wakati wa utafiti huu ilibainika kuwa Wajumbe wengi wa Kamati za Shule wanaotokana na jamii hawahusiki kikamilifu katika kutekeleza majukumu yao na hivyo walimu kulemewa na mzigo au walimu wasiokuwa waaminifu kuchukua nafasi hiyo kufuja fedha na raslimali za umma bila ya wanajamii kuwa na taarifa.

· Kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya Mapato, kuna haja ya halmashauri na serikali za vijiji viweke mpango wa kugharimia chakula, viburudisho kwa wajumbe wa Kamati za Shule wanapokuwa wanatekeleza shughuli zinazohusiana na Kamati hizo ili kuondoa uwezekano wa kushawishiwa na walimu( wanaolipwa mshahara) kukiuka ama kufanya maazimio yanayolenga kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.

· Kuna haja ya Halmashauri ya Wilaya kufanya tathimini ya MMEM na hasa ili kubaini kiwango cha ubadhilifu unaodaiwa kufanywa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.

· Ni vema halmashauri ya wilaya ya Bukoba iimarishe kitengo cha ukaguzi wa shule ili kuwawezesha wataalam wa idara na hiyo na Mhandisi wa Halmashauri kufanya ufuatiliaji wa karibu wa shule za msingi hususan kwa shule ambazo ziko mbali na makao makuu yake badala ya hali ya sasa ambapo baadhi ya shule huchukua kati ya miaka 3 hadi 5 kabla ya kutembelewa na maafisa hao.

· Kutokana na hasara iliyosababisha baadhi ya shule za msingi kutapeliwa vifaa vya ujenzi na mfanyabiashara anayedaiwa kuwa na mahusiano na baadhi ya viongozi wa Halmashauri hiyo, kuna haja ya uongozi wa juu kufanya uchunguzi wa kina juu ya madai hayo na kuwachukulia hatua wahusika.

· Ni vema miradi ya ujenzi mashuleni iwe inaibuliwa na mikutano ya vijiji husika ili vipaumbele viainishwe na jamii husika na kuifanya iwe na ari ya kuchangia maendeleo yake badala ya ilivyo sasa ambapo miradi mingi huibuliwa kwa misingi ya kisiasa.

HITIMISHO

Matokeo ya zoezi la PETS lilifanyika katika tarafa aza Rubale, Kyamtwara, Katerero na Bugabo ni mrejesho kutoka kwa jamii jinsi wanavyoiona hali halisi ya matumizi ya fedha za umma katika sekta ya elimu katika maeneo yao. Matokeo haya yanalenga kuwasaidia wadau mbalimbali, kutafakari namna ya kuyatumia katika kurekebisha upungufu unaotajwa na wapokeaji huduma ili kuziboresha na kutoa huduma kwa ufanisi zaidi. Vile vile matokeo ya zoezi hili yanakusudia kusaidia katika kuhakiki iwapo thamani ya fedha (value for money) inazingatiwa katika kuboresha utoaji wa huduma za jamii. Kwa mfano, uchunguzi unaangalia zaidi ya ujenzi wa chumba cha darasa na kusimamisha jengo kwamba vifaa vilivyotumika ni bora, thamani yake inalingana na malipo aliyopewa mkandarasi, jengo ni imara, halina nyufa, vipimo ni sahihi kadiri ya viwango vilivyoelekezwa? Mfano wa lengo hili la kubaini viwango vya bidha inayotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni umejidhihirisha katika Shule ya Katerero ambapo mbao zilizotumika kwa ajili ya kuezeka chumba cha darasa chini ya MMEM ni tofauti za zile ambazo shule ilikuwa imekubaliana na mkandarasi na matokeo yake zinawahi kuoza kwa kubunguliwa. Kama ni utengenezaji wa madawati ya wanafunzi, je vipimo ni sahihi kadiri ya viwango vinavyokubalika, aina ya ubao uliotumika ni ule unaotajwa katika mkataba, uimara unaridhisha, idadi ya dawati ni sahihi na kuna utaratibu wa kupokea vifaa kama dawati zinapowasilishwa na mkandarasi ili ikibidi zikaguliwe kwa kulinganisha na masharti ya mkataba? Hii ni baadhi ya mifano tu jinsi ya kuhakiki ili kubaini iwapo ipo mianya ya pakacha kuvuja, linavujia wapi na wahusika ni akina nani.

Mtazamo wa wananchi kuhusu zoezi la PETS ni wa kuliunga mkono na kwamba limewafumbua macho kuhusu haki yao ya kupata habari ili wazitumie katika kufuatilia matumizi ya fedha za umma. Hata hivyo, angalisho lilitolewa kuwa viongozi na watendaji kata nao wabadilike kwa kuwajibika kwa wananchi . Ilidokezwa kuwa upeo mdogo wa viongozi walio wengi ngazi ya kijiji unachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha upungufu unaojitokeza katika utendaji.

Wananchi kukubali kutoa taarifa zilizotengeneza ripoti hii ni ishara tosha kuwa wanathamini mchango wa wake katika kuboresha hali zao za maisha kupitia sekta husika.Wengine waliochangia mafanikio ni SNV ambao walimwezesha Kujenga Uwezo wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa Kagera (KPC) kuendesha zoezi hili. Kupitia taarifa hii tunapenda kuwashukuru wote kwa michango yao kwa namna mbalimbali hadi kukamilisha zoezi lenyewe.

Zoezi hili limehusisha shule 20 tu katika wilaya ya Bukoba vijijini ambayo ina shule 144. Tunaomba wadau mbalimbali waendelee kutoa ushirikiano wa dhati kwani zoezi la PETS ni endelevu. ASASI na watu binafsi waliopewa mafunzo wasaidie kuelimisha jamii namna ya kuendelea kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma siyo tu katika sekta za elimu bali pia katika sekta nyingine kadiri zitakavyopendekezwa na jamii husika ili MKUKUTA na malengo ya millennia viweze kufikiwa.

Mwisho wa kazi ya Uchunguzi