Wednesday, July 21, 2010

Kagera Press Club yapata milioni 40 kutoka TMF !


Na Mwandishi Wetu.


Chama cha Waandishi mkoa wa Kagera(KPC) kimepata jumla ya shilingi milioni 40 kutoka mfuko wa kusaidia vyombo vya habari na waandishi wa habari nchini Tanzania(TMF) .


Fedha hizo zitatumiwa na wanachama wa KPC kufanya uchunguzi na kuripoti kwenye vyombo wanavyowakilisha kuhusuaiana na masuala ya uchaguzi katika majimbo ya uchaguzi ya Bukoba mjini na Bukoba vijiini.

Waandishi hao watawezeshwa kufika katika maeneo ya vijiji,kata na kuchunguza sababu zinazosababisha wananchi kutijipokeza kwa wingi kujiandisha kwenye daftari la wapiga kura na kupiga kura katika majimbo hayo.

Viongozi wa KPC ambao ni Mwenyekiti wa Bw Gilbert Makwabe na Katibu Bw Mathias Byabato walisaini mkataba kwa ajili ya kupokea fedha hizo kwenye Ofisi za Tanzania Media Fund(TMF) Jijini Dar Es Salaam Julai 21,2010 kwa niaba ya wanachama wa KPC.



Akiongea kabla ya kusaini mkataba huo Meneja wa TMF Bw Ernest Sungura aliwapongeza wanachama wa KPC kwa kufanikiwa kupata fedha hizo na kuwa KPC imepewa fedha baada ya andiko lao kukidhi vigezo na kwamba awali watapewa asilimia 82 ya fedha hizo na asilimia 18 watapewa baada ya kukamilisha mradi huo.



Akiongea kwa niaba ya KPC Mwenyekiti wake Bw Makwabe aliishukuru TMF kwa kutoa fedha hizo na kuhaidi kufanya kazi kulingana na makubaliano yaliyopo kwenye andiko lenyewe na mkataba.



Kwa mjibu wa andiko hilo wanachama hao watalazimika kufanya kazi kwa muda wa miezi sita kuanzia Agust 2010 hadi Januari 2011.

Pichani:Katibu wa Kagera Press Club Bw Mathias Byabato (Kulia) akisaini mkataba wa kupokea shilingi milioni arobaini kutoka TMF ,Katikati ni Meneja wa TMF Bw Ernest Sungura na kushoto ni Afisa wa TMF anayehusika na masuala ya ruzuku za mashirika Bw Derek Murusuri