Kauli hizi za wanasiasa wanawake hazifai !
Wakati tunaunga mkono harakati za kutafuta usawa wa kijinsia zinazofanywa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wanaharakati, wanawake wenyewe pamoja na sisi wanaume, katu hatuungi mkono fikra zinazopandikizwa sasa kuwa wanawake ni lazima kuwachagua wanawake wenzao.
Katika awamu hii ya uongozi wa nchi unaokaribia kumaliza muda wake ukiahidi kuwa lengo
Kuwa wanawake wako upande wao halikadhalika wanaume upande wao hali inayoashiria kujenga matabaka katika nchi yetu. Hali hii haiwezi kupewa nafasi na kuachiliwa iendelee kwa kuwa itakuwa inapotosha dhana nzima ya kuwawezesha wanawake na badala yake kuifedhehesha jamii nzima.
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wapiga kura waelimishwe kumchagua kiongozi mwadilifu, anayeelewa matatizo yao, mwenye maono na ambaye ni sehemu ya jamii (‘anayekula na kuishi nao’kwa kila hali), lakini si kupiga debe achaguliwe fulani kwa sababu ya jinsi yake , kabila lake au dini yake.
Kwa hiyo tuwahamasishe wananchi wawachague viongozi bora na si kwa tofauti zao za kidini, kikabila wala kimaumbile. Hivyo yeyote atakayehamasisha watu kuwachagua wagombea kwa sababu ni wanawake na tofauti na yule anayepandikiza ubaguzi wa kidini au kikabila.
Kauli kama hizi ni maarufu
Ni mtazamo wetu kuwa kama ilivyo kwa baadhi ya wanaume, hata katika kundi la wanawake kuna wasio na upendo, wasio waaminifu, wakatili na hata majambazi. Ndiyo maana tunawasihi watanzania tumchague kiongozi kwa kuangalia uwezo na zifa alizonazo mgombea kama kiongozi bora bila kutanguliza jinsi, kuwapa nafasi wanawake kuchukuliwa kuwa ni vita au uadui kati ya wanawake na wanaume.
Kama wanawake wote wataungana kuwaunga mkono wanawake wenzao tu,mwanaume gani atapita?.
Baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wanawake walishawahi kutoa kauli za kuchefua hivi karibuni mfano, mmoja wapo ni kiongozi mmoja wa wanawake aliyekaririwa katika chombo kimoja cha habari akisema ‘’Rafiki wa mwanamke ni mwanamke’’.
Baada ya siku chache kiongozi mmoja mwanamke akiwa kwenye ziara mkoani Arusha alikaririwa akiwataka wanawake kuwa na umoja na kupendana ili waweze kuwashinda wanaume katika uchaguzi mkuu.
Haitoshi mwingine akiwa wilayani Arumeru alikaririwa na vyombo vya habari akisema, ‘’Wanawake ni jeshi kubwa wakishirikiana wanaweza kuwania na kugombea nafasi mbalimbali na kuwashinda wanaume’’.
Hofu yetu sisi Malengo Yetu ni kuwa kutokana na uwingi wa wanawake tutakuwa na bunge la wanawake, endapo kauli
Hata hivyo hatari nyingine inayoonekana ni kuwa sasa kuna kundi moja katika jamii ambalo limejipanga kuanzisha mapambano. Sasa hofu yetu inajengeka katika ukweli kuwa ni athari gani zinazoweza kujitokeza endapo kundi linaloshambuliwa katika jamii wakati wa mapambano hayo litaamua kujihami?
Pengine sio rahisi kupata jibu. Sisi Malengo Yetu tunaamini kuwa mchakato kufikia malengo ya asilimia 50 kwa 50 za wanawake na wanaume katika nafasi za maamuzi hatuhitaji kutumia lugha za kuchochea mapambano bali kutumia uhamasishaji. Wengine katika lugha sanifu zaidi wanasema tunahitaji kutumia uzengeaji na uchechemuzi( lobbying and advocacy).
Katika matumizi mabaya ya Demokrasia ipo mifano ya maamuzi ya ovyo yaliyofikiwa na kuwa na athari mbaya kwa jamii kutokana na kutumia kigezo cha wengi wape. Kwamba hata
Katika maana yake halisi Demokrasia ni kama mkondo wa maji mbayo hutiririka siku zote kutoka kileleni hadi bondeni, maji hayawezi yenyewe kupanda kilele cha mlima hadi nguvu fulani itumike.
Kwa hiyo demokrasia ya wanawake kushika nafasi za uamuzi kwa asilimia 50 kwa 50 inabidi itumike kwa busara katika uchaguzi ujao. Isije kuwa kulazimisha maji kupanda kilele cha mlima. Lengo la uchaguzi si wanawake kuwashinda wanaume bali ni kushindanisha hoja, fikira,mitazamo,maono na uwezo wa kuwa kiongozi bora wa wanaume, wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment