Friday, November 6, 2009

ZIARA YA WANACHAMA WA TABORA PRESS CLUB KWENYE PRESS CLUB YA KAGERA

Katika mradi wa Balaza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania - (MCT) na Jumuhiya ya Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (Union Of Tanzania Press Clubs), Tabora Press Club ilipata fursa ya kuitembelea Kagera Press Club iliyoko Mkoa wa Kagera. Katika Ziara hiyo pia waliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya hiyo Bw. Abubakar Kasan.

Ziara hiyo ilikuwa ya siku tano iliyolenga kubadilisha uzoefu kwa kila Klabu iliwahusisha wanachama watano kutoka Tabora Presss Club ambao ni Juma Kapipi,Salma Abdul,Chuma Shomari,Swaumu Juma na Murugwa Thomas.

Katika nasaha zake kwa wana Tabora Press na wanachama wa Kagera Press Club ,Mkurugenziwa UTPC aliviasa Vilabu vya Waandishi wa habari nchini kuwa makini katika kupanga mipango yake ya maendeleo. Amesema inabidi kuwepo ubunifu makini ikiwa lengo ni kuboresha kipato cha Wanachama wake na kukuza uchumi kwenye vilabu vyao.

Akitoa ushauri huo Bw. Karsan alisema "hakikisheni kabla ya kupitisha mradi/miradi kwanza angalieni mapato na matumizi, tengenezani mpango endelevu wa biashara na kuhakiki kwa makini sana je, mpango huo utaleta tija na ni endelevu"

alisema bila kufanya hivyo vilabu vitajikuta vinakuwa mufilisi au kuleta migogoro kwenye vilabu vyao na kwamba hali hiyo inaweza kuwa chanzo cha kusambaratisha umoja ambao tayari umekwisha kuwepo.

Alifafanua kwamba Jumuiya ya Vyama vya Waandishi wa Habari (UTPC) uhai wake ni uhai wa Press Clubs nchini na kwamba hivi sasa Pemba Press Club ndiyo inayoongoza kwa sasa kwa maendeleo kuliko press club nyingine nchini.

Karsan alito ushauri huo baada ya taarifa ya KPC iliyotolewa kwa wageni hao kufafanua kuwa miradi iliyokuwa tayari ikiiendesha na club hiyo kuwa ni pamoja na Gazeti la kila wiki liitwalo "Malengo yetu" ambalo lengo kuu ni kuhabarisha jamii ya maeneo ya kanda ya ziwa wanaishi maeneo ya vijijini ambako habari nyingi haziandikiwi au magazeti ya kitaifa kufika kwa sababu mbalimbali.

"Pamoja na miradi mingine ambayo Kagera Press Club inakusudia kuendesha ni kuwa na Chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) na tayari Chama hicho cha waandishi wa Habari kipo kwenye mchakato kwa kushirikiana na Wanajamii na Wadau mbali mbali wakiwemo UTPC,Shirika la Maendeleo laNetherland SNV kuanzisha Radio ya Kijamii (Community Radio) iitwayo "Omumwani Fm" jina hilo lilitokana na Wanajamii kwenye kikao cha pamoja kilichofanyika mjini Bukoba

Kwenye ziara hiyo ya Waandishi wa Habari kutoka Tabora (Tabora Press Club) walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali katika Wilaya ya Missenyi mpakani mwa Tanzania na Uganda na kujionea Soko kuu la Kimataifa la kuuzia mazao mbali mbali hasa ndizi zitokazo katika Mkoa wa Kagera. Soko hilo ni kiungo muhimu kwa matumizi ya Nchi zinazo jumuisha Afrika Mashariki na Kati.

Pia katika ziara hiyo walitembelea Viwanda mbali mbali, Kiwanda cha kuchapia Gazeti na Vitabu (Rumuli Printing Press) kilichoko Bunena, Kiwanda cha kukoboa Kahawa BUKOP LTD na kuonyeshwa kahawa zinavyokobolewa na walifurahia baada ya kuona kahawa zinavyokobolewa na kupata nafasi ya kukitembelea Kiwanda cha kusindika Kahawa (TANICA) na kuonyeshwa jinsi Kahawa inavyosindikwa mpaka inawekwa kwenye kopo ikiwa tayari kupelekwa kwenye masoko.

Fursa hiyo walitembelea kwenye kijiji cha Maonesho mbali mbali ya kale kinacho simamiwa na kituo cha utalii cha Kiroyera ambacho hushughulikia Utalii katika mkoa huu na Kitaifa na kujionea vivutio vilivyopo kwenye sehemu mbali mbali zilizoko Mkoani Kagera, ikiwa baadhi Nyumba za zamani za Msonge, vifaa vitumikavyo kushikia Senene,

(Senene ni kilaji maalum na kuheshimika sana katika nyanja mbali mbali katika tamaduni za Kihaya), vibuyu vya kuwekea pombe ya kienyeji (Rubisi) na kuona picha maalum zinazo onyesha ndege ambazo hazipatikani kwenye sehemu yoyote nchini, nyoka na vipepeo. Haya ni baadhi tu kwa vile kijiji hicho kina mambo mengi muhimu yamanufaa kwa kujione.

Waandishi hao kutoka Tabora Press Club, walivinjali kwenye ufukwe wa Ziwa Victoria, ziwa linalo unganisha Tanzania, Uganda na Kenya na kujionea mandhari ya Ziwa hilo na viunga vya Ziwa hilo ikiwa ni pamoja na Kituo cha Nyamkazi ambako sehemu muhimu ya kufikishia samaki kutoka ziwani na kupimwa tayari kupelekwa Viwandani. Matembezi hayo pia walikiona kwa macho yao Kisiwa kiitwacho "MUSIRA" na kuitembelea Shule ya kisasa iliyoko Kata ya Ijuganyondo ya Kemebos.

Ziara hiyo iliwachukua siku tano na mwisho Waandishi hao walihitimisha ziara yao kwa kubadilishana mawazo na uzoefu na wenyeji wao kwenye viwanja vya "Bukoba Club" iliyoko kwenye Manispaa ya Bukoba.

Tunawashukuru sana wote waliofanikisha ziara hiyo ikiwemo wale wopte waliokubali wageni wetu kutembelea ofisi maeneo yao.

Hapa Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC akiteta jambo na baadhi ya viongozi wa KPC.Yupo Method Kalikila,Gilbert Makwabe na Pontian Kaiza
Unaweza kusoma historia ya Kagera Press Club kwa kubonyeza hapa

No comments:

Post a Comment