Wednesday, January 27, 2010

Ukweli kuhusu 'Mzungu' anayecharaza wananchi viboko Kagera !

Baadhi ya waandishi wakifanya mahojiano na wakazi wa kijiji cha Ijumbi wanaoishi kwa mashka.





Licha ya kucheka lakini wanacharazwa bakora,wengine ni wazee sana


Taarifa za kuwepo raia mmoja wa kigeni anayenyanyasa wananchi zimekuwa zikiripotiwa na vyombo kadhaa vya habari lakini kagera press club iliwatuma waandishi 7 wa vyombo kadhaa kuchunguza chanzo cha mgogoro huo.


kilichobainika ni hiki hapa.


Na Mwandishi wa Blogspot

KATIKA hali isiyo ya kawaida wananchi wapatao 100 wa kitongoji cha Bujenjeke kijiji cha Ruhija kata ya Ijumbi wamekuwa waakilazimika kuhamisha makazi yao porini kukwepa kipigo kutoka wanamgambo wakishirikiana na askari polisi wanaodaiwa kununuliwa na raia wa kigeni.

JESHI la polisi mkoani Kagera limejikuta likiwa katika lindi la mgogo mkubwa kwa kile kinachodaiwa kuwa kumkingia kifua raia wa kigeni anayedaiwa kuwanyanayasa wananchi na kuwalazimu kukimbia nyumba zao na kulala vichakani zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Hayo yamebainika jana baada ya kundi la waandishi wa habari wa mkoani Kagera kulazimika kufanya ziara ya siku moja ya kwenda kuchunguza malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi ya kudai kunyanyaswa na Mzungu ambaye ni anadaiwa kuwa ni raia wa nchini Uingereza.

Wakizungumza na waandishi wa habari wakazi wa kijijini hapo, walidai kuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilala na kushinda porini, kukwepa kupigwa na askari polisi wanaodaiwa kuwa katika ofisi ya Kamanda wa polisi Mkoani Kagera na wanamgambo wanaokodishwa kutoka maeneo yaasiojulikana kutokana na mavazi wanayovaa aina ya kininja.

Katika uchunguzi uliofanywa na kundi hilo la wandishi wa habari kutoka chama cha waandishi mkoa wa Kagera(Kagera Press Club) uliweza kubaini kutokuwepo kwa dhana ya utekelezaji wa kilimo kwanza kutokana na kutokuwepo hata shamba jipya linaloonesha kulimwa hivi karibuni zaidi ya zamani kukanda, huku wananchi wakidai kuwa wanashindwa kujishughulisha na kazi za kilimo kutokana na vitisho, vipigo na kuswekwa rumande kwa kubambikiziwa kesi.

Mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Bahabti Mussa (32) alisema chanzo cha migogoro hiyo ni baaada ya mzungu huyo raia wa Uoingereza, Robert Maintland kwenda kijijini hapo, mwaka 2003 ambapo alifika na kuweka kuanza kuweka vigingi bila kuishirikisha jamii iliokuwa ikiishi hapo, na baadaye kuondoka na kurudi Uingereza.

Alisema mwaka 2008 Maintland alirejea tena nchini na baada ya siku tano kupita badhi ya wananchi walienda kumsalimia kama jirani yao, ambapo katika hali isiyo ya kawaida aliwataka waondoke katika eneo hilo.

Hata hivyo, Musa alisema kuwa walilazimika kumhoji wakiondoka wakiondoka atawalipa, ambapo aliwajibu kuwa angewalipa kuanzia sh. 100,000 hadi 350,000 na kumwambia Mussa kuwa kwa kuwa yeye ni msemaji sana angweweza kumlipa sh. 500,000 kitu ambacho wanchi hao hawakuweza kuafikiana naye, ambapo aliwaambia kuwa asiyeafikiana naye atakipata cha 'moto'.

Naye Elenestina Eleneus (74) alisema yeye kutokana na kutokuwa na nguvu anapata shida kwa kipindi kwa vurugu na vitisho vinavyofanywa askari hivyo amekuwa akishinda vichakani ili kunusuru uhai wake.

Alisema tangu uhai wake hajawahi kushuhudia hali hiyo hapa nchini hasa katika kitongoji hicho.
Alisema kwa sasa hata vifaa vyajke vya kupikia vimsombwa na askari hao na kwenda navyo kusikojulikana na hivyo kulazimika kulia kwenye majani ya migomba.

Jenipha Romwad (29) alidai Novemba 2, 2008 saa 2 asubuhi alipata kipigo kikali kutoka kwa askari akiongozwa na mwanagambo mmoja aliyemtambua kwa jina moja la James huku mzungu akivurumisha risasi kadhaa hewani ya kuwatishia ulifanya mimba yake miezi minane kutoka na kufariki, pamoja na maumivu hayo alisondekwa rumande siku mbili katika kituo cha Muleba kwa madai kuwa ni wavamizi wa ardhi ya Mzungu.

"Nikiwa na mtoto wa mwingine, nilipigwa teke la kiunoni na tumboni na huyo askari hadi kusababisha mimba yangu ya miezi minane kutoka, cha kushanga pamoja na ugonjwa wangu wala polisi pale Muleba hawakunijali hata kunipa huduma na hata sijui kichanga alikozikwa wala hata jinsi yake"alisema.

Mzee Kasenene (80) anayedaiwa kuwa alikuwa mpishi wa mmiliki wa shamba hilo aliyejulikana kwa jina la Peter Pantelakis alisema kwamba wamekuwa wakiishi kwa matesho makubwa kutoka na uwepo wa raia huyo wa kigeni.

Kwa upande wa Mzungu Robert Maintland ambaye hakuwepo katika eneo hilo akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu, alisema kuwa ardhi yake na hakuna hata raia wa Tanzania anayeishi pale kwani wote ni Warundi waliokuwa vibarua wa babu yake.

"Hakuna hata mtu wa Mtanzania nayeishi katika eneo lile, wote ni Warundi, ambao wanatabia mbaya za kubaka kuua,wakata miti ovyo"alisema.

Hata hivyo, Maintlanda alidai watu hao wanatumwa na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Wilson Masuilingi kuendeela kusihi karika ardhi yake ili aendelee kupata wapiga kura wengi.

Kuhusu kuwavamia na kuwapiga wananchi kulazimika kuhama makazi yao kwa kushirikiana na askari na wanamgambo anaowakodi kutoka katika maeneo yasojulikana, alikataa na kusema kuwa yeye hajui na wala hajui kufanya hivyo na kwamba hayo ni majungu anayopikiwa juu yake ya kumpaka matope.

Halikadhalika kuhusu kuwazuia wananchi kuchukua aina yoyote ya mazao kutoka kwenye msitu unaowanguka, mazao kuvuna mazao waliolima na hata kulima na kutumia maji ya Kurumiyo yalioko katika kitongoji hicho kwa matumizi ya nyumbani alidai kuwa hakuwahi na kwamba yote hayajui.

Mbunge wa Jimbo la Kusini, Masilingi akuzunguzia sakata hilo, alikiri kupokea taarifa za malalamiko ya manyanyaso waofanyiwa wananchi hao na huyo raia wa Kigeni na kufanya mikutano wa hadhara katika kitongoji hicho akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muleba, Angelina Mabula ambapo waliagiza raia huyo wa kigeni akamatwe na kuchukuliwa hatua, lakini anashangaa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwake.

Alisema wananchi walitakiwa kubaki katika kitongoji chao na kuendelea na shughuli zao kama wananchi wa kawaida.

Alisema katika suala nzima ya Kitingoji hicho kutaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kuingilia kati na kuchunguza mgogoro wake ambao umegubikwa na harufu za rushwa.

Alisema mzungu huyo anataka kumiliki kitongoji kizima wakazi wakazi hao waliwepo katika eneo hilo miaka mingi, na kwamba katika eneo hilo kuna mgogo wa wanafamilia baina ya mzungu na ndugu zake, mgogoro ambao wananchi hawahusiki kabisa.

Kuhusu ujenzi wa vigingi alisema kuwa unatokana na maafisa wa ardhi kula rushwa, kwani ujenzi huo haujahusisha wakazi wa eneo lile, kwa nini ijengwe vigingi wakati serikali.

Naye Kamanda wa polisi Mkoa Kagera Bw Henery salewi alipotakiwa na waandfishi wa habari kuelezea juu ya mgogoro huo unaodaiwa kuwa polisi wake ndiyo wamekuwa wakitumiwa na mzungu huyo kwenda katika kitongoji kuwatishia wananchi na kuwapora mali zao huku wenginew akiwapiga hadi kuharibiwa kwa mimba zao , alikataa kuonana hata kuzungumza na waandishi wa habari na kuwataka waandishi hao wamuulize mkuu wa mkoa ambaye hakuweza kupatikana mara moja.

"Ninashughuli nyeti, kama mtakataka kushuhudia njooni kwa Mkuu wa Mkoa, au nendeni mkaongee naye atawapa jibu"alisema licha ya waandishi wa habari kufika ofisini kwake jana saa 4. asubuhi na kuwajibu kupitia msaidizi wake kuwa tumpigie simu saa nane mchana ili aaweze kutuambia yuko wapi tuweze kuzungumza naye.

Eneo linalogombaniwa na mzungu na wananchi hao mwanzoni kabla ya uhuru lilikuwa na ukubwa wa hekari 900 na baadaye hekari zaidi ya 200 ziligawiwa kwa wananchi na kubaki hekari 741.34 ambapo ardhi hiyo ilipimwa mwaka Septemba 15, mwaka 1927 na kugawawia wananchi mwaka 1961.

vyombo vingine vilivyochapisha habari za raia huyo ni tanzania daima na Channel ten tv

No comments:

Post a Comment