Thursday, January 7, 2010

Waandishi tuweni makini kipindi cha lawama kwetu kimekwisha anza !



Wapendwa wanachama wa Kagera Press Club wanaofuatilia taarifa kama hizi kupitia blog hii na hasa waliko nje ya Manispaa ya Bukoba tunawaomba na kuwatahadharisha sana kuwa makini katika shuguli zao za kila siku za kuhabarisha jamii hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

mfano tazama taarifa kama hii hapo juu iliyotolewa na CCM Bukoba mjini,ni taarifa nzuri lakini yenye kuitaji uangalizi mkubwa wakati wa kuandika stori kutoka kwenye taarifa hiyo kwa kutazama taratibu za kupata wagombea wa vyama,mapenzi ya watu nk.

Tumeweka taarifa hii si kwa lengo la kuibeza bali kuwalewesha kwamba kupitia taarifa hii waandishi wanaweza kulisha wananchi umbea,au kutumika kama kasuku tu.

Hata hivyo tunachukua nafasi hii kuwapongeza redio Kasibante Fm ya mjini bukoba kwa jinsi ilivyotanagaza habari hiyo (ya jana saa 3:00 usiku) kutoka kwenye taarifa hii na kuwaomba waandishi wengine ambao ni wanachama wa Kagera Press Club kuiga mfano wa uhariri uliofanywa na wahariri wa redio hiyo.

Tofauti na hapo waandishi tutaendelea kuwa 'makasuku' tu na kutumiwa na vyama badala ya kuchambua hoja kuhusu yale wanayotueleza na mwisho wake ni kupotosha jamii ambayo inakosa umakini katika kuchagua viongozi wanaowafaa na wenye kuwaletea tija.

Imetolewa na Uongozi
Kagera Press Club
Januari 7,2009

No comments:

Post a Comment